Hamia kwenye habari

Kuanzia kushoto hadi kulia, safu ya juu: Ndugu Vladimir Kochnev na mke wake, Galina; Ndugu Vladislav Kolbanov. Safu ya chini: Ndugu Pavel Lekontsev na mke wake, Oksana; Ndugu Sergey Logunov na mke wake, Larisa; Ndugu Nikolay Zhugin na mke wake, Galina

OKTOBA 1, 2021
URUSI

Ndugu Watano Wameazimia Kuvumilia Licha ya Mateso

Ndugu Watano Wameazimia Kuvumilia Licha ya Mateso

Mfuatano wa Matukio

  1. Mahakama ya Wilaya ya Industrialniy iliyoko Orenburg itatangaza hivi karibuni uamuzi katika kesi inayohusu Ndugu Vladimir Kochnev, Ndugu Vladislav Kolbanov, Ndugu Pavel Lekontsev, Ndugu Sergey Logunov, na Ndugu Nikolay Zhugin. a Mwendesha-mashtaka bado hajatoa ombi la hukumu anayopendekeza

  2. Machi 1, 2021

    Zaidi ya mwaka mmoja baada ya kesi hiyo kurudishwa kwenye ofisi ya mwendesha-mashtaka, kesi ilianza kusikilizwa katika Mahakama ya Wilaya ya Industrialniy iliyoko Orenburg

  3. Januari 14, 2020

    Kesi ya uhalifu ilirudishwa kwenye ofisi ya mwendesha-mashtaka kwa sababu mashtaka hayakuwa wazi

  4. Agosti 3, 2018

    Vladimir aliachiliwa kutoka mahabusu baada ya siku 79 na akawekwa chini ya kifungo cha nyumbani

  5. Mei 16, 2018

    Wenye mamlaka walifanya upekuzi katika nyumba za familia 19 katika Eneo la Orenburg. Vladimir na Vladislav walipelekwa mahabusu. Vladislav aliwekwa chini ya kifungo cha nyumbani siku tatu baadaye

  6. Mei 14, 2018

    Msimamizi wa Kamati ya Uchunguzi ya Shirikisho la Urusi katika Eneo la Orenburg alifungua kesi ya uhalifu dhidi ya ndugu wote watano

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Hata ingawa kesi dhidi ya imani yao imeendelea kwa zaidi ya miaka mitatu, ni wazi kwamba ndugu zetu wapendwa wameazimia kudumisha ushikamanifu wao kwa Yehova. Ni wazi pia kwamba Yehova anatenda kwa ushikamanifu kuwaelekea.—2 Samweli 22:26.

a Tarehe ya hukumu haitolewi mapema pindi zote