Hamia kwenye habari

Kushoto hadi kulia: Ndugu Viktor Bachurin, Aleksandr Kostrov, na Artur Netreb

APRIL 27, 2021
URUSI

Ndugu Watatu Kutoka Lipetsk Wafikishwa Mahakamani kwa Sababu ya Imani Yao Baada ya Siku 331 Mahabusu

Ndugu Watatu Kutoka Lipetsk Wafikishwa Mahakamani kwa Sababu ya Imani Yao Baada ya Siku 331 Mahabusu

HABARI ZA KARIBUNI | Mahakama ya Urusi Yakataa Rufaa

Januari 20, 2022, Mahakama ya Eneo la Lipetsk ilikataa rufaa ya Ndugu Viktor Bachurin, Ndugu Aleksandr Kostrov, na Ndugu Artur Netreba. Watahitajika kulipa faini zao

Novemba 24, 2021,Mahakama ya Wilaya ya Sovetskiy huko Lipetsk iliwahukumu Ndugu Viktor Bachurin, Ndugu Aleksandr Kostrov, na Artur Netreba na ikawapiga faini ya rubo 500,000 (dola 6,700 za Marekani) kila mmoja. Hata hivyo, wanahitaji tu kulipa rubo 300,000 (dola 4,000 za Marekani) kwa kuwa mahakama inawapunguzia gharama kwa sababu ya muda waliokuwa mahabusu. Hawahitaji kwenda gerezani.

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Viktor Bachurin

  • Alizaliwa: 1962 (Pavlovsky Posad, Eneo la Moscow)

  • Maisha Yake: Amefunga ndoa, ana watoto wawili na mjukuu mmoja wa kike. Alianza kujifunza Biblia na Mashahidi wa Yehova mapema katika miaka ya 1990 na akabatizwa mnamo 1992. Kwa sasa, yeye peke yake ndiye Shahidi katika familia yake

Aleksandr Kostrov

  • Alizaliwa: 1961 (Sortavala, Jamhuri ya Karelia)

  • Maisha Yake: Alifanya kazi akiwa rubani, mchomelea vyuma kwa kutumia gesi na umeme, na pia akiwa fundi umeme. Alifunga ndoa na Larisa mwaka wa 1997. Wana watoto wawili. Sasa amestaafu na anapenda kuvua samaki. Alibatizwa katika mwaka wa 2002 baada ya kutambua umuhimu wa kuishi maisha yanayotegemea kweli za Biblia

Artur Netreba

  • Alizaliwa: 1978 (Glodeni, Moldova)

  • Maisha Yake: Alifunga ndoa na Svetlana katika mwaka wa 1995 na ana binti mmoja. Familia yao ilihamia Lipetsk ili kutafuta kazi. Anafanya kazi akiwa meneja wa mauzo. Alisadikishwa kwamba kutumia kanuni za Biblia kunamsaidia mtu kuwa na kusudi halisi maishani. Alibatizwa mwaka wa 2000

Historia ya Kesi

Desemba 2, 2019, wenye mamlaka katika Eneo la Lipetsk walivamia nyumba saba. Ndugu Viktor Bachurin, Ndugu Aleksandr Kostrov, na Ndugu Artur Netreba walikamatwa. Idara ya Usalama wa Taifa (FSB) iliwashtaki kwa kushiriki “uhalifu mbaya zaidi dhidi ya katiba” kwa sababu tu walihudhuria mikutano ya kutaniko na kushiriki utendaji mwingine unaohusiana na ibada yao. Ndugu hao waliwekwa mahabusu kwa siku 331.

Aleksandr anasema kwamba uhusiano wake na Yehova uliimarika zaidi alipokuwa kizuizini: “Wakati wa majaribu kama haya, unatambua kwamba chanzo kikuu cha msaada ni Yehova.”

Artur anasema hivi kuhusu mambo aliyoazimia: “Nimeazimia sitapoteza shangwe yangu wala mtazamo wangu mzuri. Ninajaribu kujikumbusha kwamba mambo yote haya ni ya muda na kwamba Baba yangu atanifariji kikweli. Popote nitakapokuwa, kuna nafasi za kuzungumza kumhusu Mungu wetu mtakatifu, Yehova.”

Viktor anaeleza: “Yehova alijifunua kwangu kuwa rafiki wa karibu sana nilipokuwa nikikabili hali hizi za pekee. Kila wakati nilihisi urafiki wa Yehova.”

Viktor anawashukuru sana ndugu na dada wote waliomsaidia mke wake ambaye si Shahidi wakati ambapo yeye alikuwa kizuizini. Viktor anasema hivi: “Mke wangu amevutiwa sana msaada ambao dada fulani wamempa. Ninasadiki kwamba watu wa familia yangu wamepata ushahidi mzuri kuhusu upendo uliopo kati ya watu wa Yehova.”

Tunajua kwamba Yehova ataendelea kuwafariji ndugu zetu wote nchini Urusi na katika nchi nyingine ambapo wanakabili mateso.​—Isaya 51:12.