Hamia kwenye habari

Kushoto: Ndugu Anton Kuzhelkov na mke wake, Alyona; Kulia: Ndugu Nikolay Prokhorov na mke wake, Yelena

JANUARI 27, 2022
URUSI

Ndugu Wawili Wauona Mkono wa Yehova na Kuendelea Kuwa Jasiri

Ndugu Wawili Wauona Mkono wa Yehova na Kuendelea Kuwa Jasiri

Mahakama ya Wilaya ya Kirsanovskiy katika Eneo la Tambov itatangaza uamuzi wake hivi karibuni katika kesi inayowahusu Ndugu Anton Kuzhelkov na Nikolay Prokhorov. Mwendesha-mashtaka bado hajatoa hukumu anayopendekeza.

Mfuatano wa Matukio

  1. Desemba 21, 2020

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Anton na Nikolay kwa sababu ya kupanga utendaji wa shirika lenye msimamo mkali

  2. Desemba 24, 2020

    Wapelelezi walifanya upekuzi katika maeneo 19 kutia ndani nyumba ya Anton. Alipelekwa eneo lililo umbali wa kilomita 350 kutoka nyumbani kwake ili kuhojiwa. Nikolay alihojiwa kisha akaamriwa asiondoke katika eneo hilo

  3. Desemba 25, 2020

    Anton hakuruhusiwa kurudi nyumbani, alipelekwa mahabusu

  4. Agosti 30, 2021

    Anton alihamishwa na kuzuiliwa kwenye kituo kingine

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tuna uhakika kwamba Yehova ataendelea kuwapa ujasiri na kuwategemeza ndugu na dada zetu wanaokabili mateso.​—Methali 1:33.

a Ndugu Kuzhelkov kwa sasa yuko mahabusu. Haikuwezekana kuzungumza naye.