Hamia kwenye habari

FEBRUARI 18, 2020
URUSI

Ndugu Yevgeniy Aksenov Ahukumiwa Kuwa Mhalifu na Kupewa Kifungo cha Nje cha Miaka Miwili Nchini Urusi

Ndugu Yevgeniy Aksenov Ahukumiwa Kuwa Mhalifu na Kupewa Kifungo cha Nje cha Miaka Miwili Nchini Urusi

Februari 18, 2020, Mahakama ya Wilaya ya Zheleznodorozhniy iliyo huko Khabarovsk nchini Urusi, ilimhukumu Ndugu Yevgeniy Aksenov na kumpa kifungo cha nje cha miaka miwili. Ikiwa kwa kipindi hiki cha miaka miwili Ndugu Yevgeniy Aksenov atahama mahali anapoishi au kupatikana na hatia ya kitendo chochote cha kihalifu, atapelekwa gerezani. Kwa kipindi cha miezi sita ya kwanza ya kifungo chake, atakuwa chini ya masharti fulani na lazima aripoti katika kituo cha polisi kila mwezi. Vilevile, katika kipindi chote akiwa chini ya masharti hayo, haruhusiwi kusafiri au kutoka nje ya mji wa Khabarovsk na pia haruhusiwi kutoka nyumbani jioni. Ndugu  Aksenov atakata rufaa ya uamuzi huo.