Hamia kwenye habari

Ndugu Yevgeniy Sokolov

JULAI 15, 2024
URUSI

Ndugu Yevgeniy Sokolov Amehukumiwa Kuwa na Hatia Katika Kesi ya Pili ya Uhalifu

Ndugu Yevgeniy Sokolov Amehukumiwa Kuwa na Hatia Katika Kesi ya Pili ya Uhalifu

Mei 29, 2024, Mahakama ya Wilaya ya Zeyskiy katika Eneo la Amur ilimhukumu Ndugu Yevgeniy Sokolov kifungo cha nje cha miaka mitatu. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Hii ilikuwa kesi ya pili ya uhalifu iliyofunguliwa dhidi ya Yevgeniy. Kesi ya kwanza, ambayo inawahusu ndugu wengine tisa, bado inaendelea katika jiji la Voronezh, ambako sasa Yevgeniy anaishi.

Yevgeniy anasema hivi kuhusu kinachomsaidia kuvumilia: “Ninajifunza kumtumaini na kumtegemea Yehova kikamili zaidi. Hatuwezi kutatua tatizo lolote kwa njia nzuri zaidi kuliko Yehova anavyoweza. Sikuzote yeye ndiye mwenye ustadi na hekima zaidi.”

Kama Yevgeniy, sisi na tuendelee kumwambia Yehova hivi: “Wewe ni kimbilio langu,” tukiwa na uhakika kwamba sikuzote atatuandalia msaada tunaohitaji.​—Zaburi 142:5.

Mfuatano wa Matukio

  1. Desemba 15, 2022

    Kesi ya pili ya uhalifu yafunguliwa dhidi ya Yevgeniy bila yeye kujua

  2. Septemba 22, 2023

    Yevgeniy apata habari kuhusu kesi ya pili ya uhalifu dhidi yake. Anahojiwa na kushtakiwa kwa kosa la “kutayarisha na kuongoza mikutano ya kidini”

  3. Aprili 22, 2024

    Kesi ya uhalifu yaanza kusikilizwa

  4. Mei 29, 2024

    Anahukumiwa kifungo cha nje cha miaka mitatu