Hamia kwenye habari

Ndugu Yevgeniy Spirin akiwa kizimbani

JULAI 9, 2020
URUSI

Ndugu Yevgeniy Spirin Anakabili Kifungo cha Miaka Saba Nchini Urusi

Ndugu Yevgeniy Spirin Anakabili Kifungo cha Miaka Saba Nchini Urusi

Mahakama ya Jiji la Furmanovsky katika Eneo la Ivanovo inaweza kutangaza uamuzi wake Julai 14, 2020, katika kesi inayomhusu Ndugu Yevgeniy Spirin. Mwendesha-mashtaka ameomba kwamba Ndugu Spirin afungwe kifungo cha miaka saba gerezani.

Ndugu Spirin mwenye umri wa miaka 34, ameshtakiwa kwa kosa la kupanga shughuli zenye msimamo mkali. Kesi hiyo ilifunguliwa na mpelelezi wa FSB Januari 21, 2019. Siku sita baadaye, maofisa wa FSB walivamia nyumba ya Ndugu Spirin na mke wake, Natalya. Mahakama ya Wilaya ya Oktyabrsky katika Eneo la Ivanovo iliagiza kwamba Ndugu Spirin awekwe kizuizini kwa angalau miezi miwili, kwa sababu tu alikuwa Shahidi wa Yehova. Muda wake wa kukaa kizuizini uliongezwa baadaye.

Julai 5, 2019, alitolewa kizuizini baada ya siku 160 na kuwekwa katika kifungo cha nyumbani. Desemba 18, 2019, Mahakama ya Wilaya ya Oktyabrsky katika Eneo la Ivanovo iliagiza Ndugu Spirin aachiliwe licha ya kwamba wapelelezi walipinga uamuzi huo. Hakuwekewa vizuizi vingine.

Tunasali tukiwa na uhakika kabisa kwamba Baba yetu mwenye upendo, Yehova, ataendelea kuwa na ndugu zetu nchini Urusi ambao wanaendelea kuteswa kwa sababu ya imani yao.—1 Petro 4:14.