Hamia kwenye habari

Kushoto hadi kulia: Ndugu Aram Danielyan, Denis Kuzyanin, Sergey Polosenko, na Nikolay Vasiliyev

DESEMBA 14, 2023
URUSI

“Siri Ni Kumtegemea Yehova”

“Siri Ni Kumtegemea Yehova”

Mahakama ya Wilaya ya Samarskiy iliyoko Samara itatangaza uamuzi wake katika kesi kuwahusu Ndugu Aram Danielyan, Denis Kuzyanin, Sergey Polosenko, na Nikolay Vasiliyev. Mwendesha mashtaka bado hajatoa ombi la hukumu anayopendekeza.

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunasadiki kwamba Yehova ataendelea kufariji mioyo ya wote wanaoteseka kwa ajili ya imani yao anapoendelea “kuwaimarisha katika kila tendo na neno jema.”​—2 Wathesalonike 2:16, 17.

Mfuatano wa Matukio

  1. Desemba 14, 2021

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Denis, Nikolay, na Sergey

  2. Desemba 15, 2021

    Nyumba za Denis, Nikolay, na Sergey zilifanyiwa upekuzi. Walikamatwa na kupelekwa kizuizini

  3. Desemba 16, 2021

    Denis, Nikolay, na Sergey walihamishiwa mahabusu

  4. Januari 6, 2022

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Aram. Alikamatwa kwenye uwanja wa ndege

  5. Januari 7, 2022

    Aram alipelekwa mahabusu

  6. Desemba 12-14, 2022

    Ndugu wote wanne walifunguliwa kutoka mahabusu na kuwekewa vizuizi vya kusafiri

  7. Juni 16, 2023

    Kesi ya uhalifu inaanza