Hamia kwenye habari

Ndugu Ivan Shulyuk

FEBRUARI 16, 2022
URUSI

Subira Inamsaidia Ndugu Ivan Shulyuk Kuvumilia Mateso

Subira Inamsaidia Ndugu Ivan Shulyuk Kuvumilia Mateso

Mahakama ya Jiji la Nazarovskiy katika Eneo la Krasnoyarsk hivi karibuni itatangaza katika kesi inayomhusu Ndugu Ivan Shulyuk. Mwendesha-mashtaka bado hajatuma ombi la hukumu anayopendekeza.

Mfuatano wa Matukio

  1. Juni 18, 2020

    Maofisa wa usalama walivamia nyumba ya akina Shulyuk na kumkamata Ivan. Aliwekwa kizuizini

  2. Juni 19, 2020

    Mahakama iliagiza Ivan ahamishiwe mahabusu

  3. Julai 9, 2020

    Aliachiliwa kutoka mahabusu. Hakuruhusiwa kuwasiliana na mtu yeyote nje ya nyumba yake bila idhini. Aliagizwa asiondoke nje ya nyumba yake kati ya saa 12:00 alfajiri na saa 5:00 usiku, hilo lilimzuia asifanye kazi

  4. Agosti 14, 2020

    Mpelelezi alijaribu kuongeza vizuizi lakini kwa sababu ya sifa nzuri ya Ivan, ombi lake lilikataliwa. Vizuizi vingi viliondolewa

  5. Agosti 17, 2020

    Aliwekewa vizuizi vya kusafiri

  6. Septemba 15, 2021

    Kesi ya uhalifu ilianza

Maelezo Mafupi Kumhusu

Tunashukuru sana kwamba “Yehova anajua jinsi ya kuwakomboa kutoka kwenye jaribu watu wenye ujitoaji-kimungu.”​—2 Petro 2:9.