Hamia kwenye habari

MACHI 25, 2020
URUSI

Uamuzi wa Kwanza Kubatilishwa Nchini Urusi, Ndugu Alushkin na Wengine Watano Washinda Kesi ya Rufaa

Uamuzi wa Kwanza Kubatilishwa Nchini Urusi, Ndugu Alushkin na Wengine Watano Washinda Kesi ya Rufaa

Machi 25, 2020, Mahakama ya Mkoa wa Penza ilibatilisha kifungo cha Ndugu Vladimir Alushkin, Vladimir Kulyasov, Andrey Magliv, na Denis Timoshin, kutia ndani Dada Tatyana Alushkina na Galiya Olkhova. Kesi hizo zimerudishwa zikasikilizwe upya.

Kwa sababu ya kushinda kesi ya rufaa, Ndugu Alushkin ataachiliwa kutoka gerezani katika siku zijazo. Yeye na wengine wataendelea kuwa chini ya vizuizi vya usafiri na vizuizi vingine wanaposubiri kesi yao isikilizwe upya.