Hamia kwenye habari

Ndugu Dmitriy Terebilov kabla ya kukamatwa. Picha ndogo: Dmitriy akiwa kizimbani alipofikishwa mahakamani

JULAI 12, 2023
URUSI

Urusi Yamshtaki Dmitriy Terebilov Kuwa Mhalifu kwa Kuzungumzia Biblia na Mfungwa Mwenzake

Urusi Yamshtaki Dmitriy Terebilov Kuwa Mhalifu kwa Kuzungumzia Biblia na Mfungwa Mwenzake

Aprili 20, 2023, wenye mamlaka nchini Urusi walifungua kesi mpya dhidi ya Ndugu Dmitriy Terebilov, ambaye amefungwa gerezani tangu Septemba 2021 kwa sababu ya imani yake. Tangu mwaka wa 2017 Mahakama Kuu ilipowapiga marufuku Mashahidi wa Yehova, hii ndiyo mara ya kwanza kwa Shahidi wa Yehova aliyefungwa gerezani nchini Urusi kushtakiwa kuwa mhalifu kwa sababu ya kuzungumzia Biblia na mfungwa mwenzake. Ikiwa Dmitriy atapatwa na hatia ya mashtaka haya mapya, anaweza kufungwa miaka nane zaidi gerezani kuongezea kifungo cha sasa cha miaka mitatu.

Kadiri mateso nchini Urusi yanavyozidi kuongezeka, uhakika wetu unazidi kuimarika kwamba Yehova ataendelea kuwapa ndugu na dada zetu nchini Urusi “nguvu zinazopita zile za kawaida.”​—2 Wakorintho 4:7.