MEI 24, 2022
URUSI
Wako Imara Licha ya Kuhukumiwa Huko Sochi
Machi 28, 2022, Mahakama ya Wilaya ya Khostinskiy iliyo Sochi ilitangaza uamuzi wake katika kesi inayowahusu Ndugu Vladimir Deshko, Ndugu Yuriy Loginskiy, Ndugu Yuriy Moskalev, na Dada Tatyana Velizhanina. Ndugu Deshko alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na miezi minne gerezani naye Dada Velizhanina alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na miezi mitano gerezani. Wote wawili tayari wametumikia vifungo vyao kwa sababu walikaa mahabusu kwa zaidi ya mwaka mmoja, hivyo hawahitaji kwenda gerezani kwa sasa. Ndugu Loginskiy na Ndugu Moskalev walihukumiwa kifungo cha nyumbani cha miaka miwili kila mmoja. Hawahitaji kwenda gerezani kwa sasa.
Mfuatano wa Matukio
Machi 24, 2021
Wote wanne walikamatwa na kuwekwa kizuizini kwa muda. Walishtakiwa kwamba walishiriki katika utendaji wa shirika lenye msimamo mkali
Machi 26, 2021
Ndugu Deshko na Dada Velizhanina walipelekwa mahabusu iliyo umbali wa kilometa 400. Ndugu Loginskiy na Ndugu Moskalev waliwekwa katika kifungo cha nyumbani
Februari 3, 2022
Ndugu Deshko aliachiliwa kutoka mahabusu na akawekwa katika kifungo cha nyumbani
Machi 3, 2022
Kesi ya uhalifu ilianza
Machi 4, 2022
Dada Velizhanina aliachiliwa kutoka mahabusu na akawekwa katika kifungo cha nyumbani
Maelezo Mafupi Kuwahusu
Tunajua kwamba Yehova ataendelea kuimarisha na kuwategemeza watumishi wake waaminifu, na kuwapa kila kitu wanachohitaji ili kuvumilia siku hizi ngumu za mwisho.—Zaburi 89:21.