Hamia kwenye habari

Safu ya juu, kushoto hadi kulia: Ndugu Aleksandr Ketov; Ndugu Andrey Kharlamov na mke wake, Larisa; Ndugu Aleksandr Kruglyakov

Safu ya chini, kushoto hadi kulia: Dada Lidiya Nekrasova; Ndugu Sergey Ushakhin

AGOSTI 10, 2023
URUSI

Wameazimia Kuwa na Shangwe Licha ya Mateso

Wameazimia Kuwa na Shangwe Licha ya Mateso

Mahakama ya Jiji la Syktyvkarskiy iliyo katika Jamhuri ya Komi itatangaza hivi karibuni uamuzi wake katika kesi inayowahusu Ndugu Aleksandr Ketov, Ndugu Andrey Kharlamov, Ndugu Aleksandr Kruglyakov, Dada Lidiya Nekrasova, na Ndugu Sergey Ushakhin. Mwendesha-mashtaka bado hajatoa ombi la hukumu anayopendekeza.

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Kama tulivyoona kwenye masimulizi haya Yehova huwapa ndugu na dada zetu “uwezo kamili” ili waweze kuvumilia majaribu na kubaki waaminifu.​— Isaya 40:29.

Mfuatano wa Matukio

  1. Machi 2, 2021

    Nyumba 14 za Mashahidi wa Yehova zilifanyiwa msako jijini Syktyvkar. Aleksandr Ketov, Andrey Kharlamov, na Aleksandr Kruglyakov walipelekwa kizuizini. Lidiya Nekrasova na Sergey Ushakhin waliwekewa vizuizi vya kusafiri

  2. Machi 3, 2021

    Aleksandr Ketov na Andrey Kharlamov waliachiliwa kutoka kizuizini na kuwekwa chini ya kifungo cha nyumbani. Aleksandr Kruglyakov alipelekwa mahabusu

  3. Aprili 27, 2021

    Andrey Kharlamov aondolewa kifungo cha nyumbani

  4. Aprili 28, 2021

    Aleksandr Ketov aondolewa kifungo cha nyumbani, na Aleksandr Kruglyakov aachiliwa kutoka mahabusu

  5. Aprili 19, 2022

    Kesi ya uhalifu yaanza

  6. Juni 9, 2022

    Hakimu alisema kesi hiyo haina ushahidi wa kutosha na akairudisha kwa mwendesha-mashtaka

  7. Februari 14, 2023

    Kesi hiyo yaanza kusikilizwa tena na hakimu mwingine