FEBRUARI 9, 2024
URUSI
Wanakabiliana na Majaribu Huku Wakimtumaini Yehova
Mahakama ya Jiji la Blagoveshchensk iliyo katika Eneo la Amur itatangaza uamuzi wake hivi karibuni katika kesi inayowahusu Dada Kristina Golik, Dada Yekaterina Olshevskaya, Dada Mariya Myasnikova, na Dada Valentina Yermilova. Mwendesha mashtaka bado hajatoa ombi la hukumu anayopendekeza.
Maelezo Mafupi Kuwahusu
Tunamshukuru Yehova kwa vielelezo ambavyo dada hawa wanatuwekea. Na tunajua kwamba Yehova ataendelea kuwatunza na kuwabariki.—Zaburi 27:3.
Mfuatano wa Matukio
Julai 20, 2018
Nyumba zilifanyiwa msako
Julai 22, 2021
Dada wote wanne walishtakiwa kuwa wahalifu
Julai 27, 2021
Kristina na Mariya waliwekewa vizuizi vya kusafiri
Agosti 3, 2021
Yekaterina aliwekewa vizuizi vya kusafiri
Agosti 4, 2021
Valentina aliwekewa vizuizi vya kusafiri
Mei 26, 2023
Kesi ya uhalifu ilianza