Hamia kwenye habari

Ndugu Sergey Rayman na mke wake, Valeriya

SEPTEMBA 7, 2020
URUSI

Wenzi wa Ndoa Vijana Wanakabili Mashtaka ya Uhalifu Nchini Urusi

Wenzi wa Ndoa Vijana Wanakabili Mashtaka ya Uhalifu Nchini Urusi

Hukumu Inatarajiwa

Septemba 16, 2020, a Mahakama ya Wilaya ya Sverdlovskiy iliyo katika jiji la Kostroma inapanga kutoa hukumu ya kesi dhidi ya Ndugu Sergey Rayman na mke wake, Valeriya. Kila mmoja wao anakabili kifungo cha nje cha miaka saba.

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Sergey Rayman

  • Tarehe ya Kuzaliwa: 1996 (Kineshma, Eneo la Ivanovo)

  • Maisha Yake: Alisomea kazi ya ujenzi katika chuo cha ufundi. Akawa mtaalamu wa kupamba upande wa ndani wa majengo wakati wa ujenzi. Alijifunza kuipenda na kuiheshimu Biblia kutoka kwa nyanya yake. Alifunga ndoa na Valeriya katika mwaka wa 2015. Anapenda kupika na kuteleza kwenye barafu

Valeriya Rayman

  • Tarehe ya Kuzaliwa: 1993 (Sharya, Eneo la Kostroma)

  • Maisha Yake: Baba yake alikufa akiwa na umri wa miaka kumi. Alijifunza kumhusu Yehova kutoka kwa mama yake. Ana leseni ya ususi

Historia ya Kesi

Mapema asubuhi Julai 25, 2018, polisi waliokuwa na silaha walitumia nondo kuvunja mlango wa nyumba ya Ndugu na Dada Rayman. Maofisa hao waliwakamata wenzi hao wa ndoa. Dada Rayman alikaa mahabusu kwa siku mbili. Ndugu Rayman alikaa siku 59 katika kifungo cha upweke. Wenye mamlaka wamewazuia Ndugu na Dada Rayman wasiwasiliane na Mashahidi wengine wa Yehova. Pia, hawaruhusiwi kutoka nyumbani jioni. Hali hiyo yenye mkazo imeathiri afya yao kimwili na kihisia.

Wenzi hao wa ndoa vijana wanaposubiri uamuzi wa kesi yao, tunasali kwamba wataendelea kuwa jasiri na wenye nguvu, wakitumaini kwamba Yehova hataacha kuwategemeza.—Yoshua 1:9.

a Inaweza kubadilishwa