Hamia kwenye habari

Kushoto hadi kulia: Ndugu Andrey Andreyev, Ndugu Artem Bagratyan na mke wake, Alevtina, na Ndugu Andrey Ryshkov

MACHI 16, 2021
URUSI

Wenzi wa Ndoa na Ndugu Wengine Wawili Wanaweza Kufungwa kwa Imani Yao Katika Eneo la Kursk

Wenzi wa Ndoa na Ndugu Wengine Wawili Wanaweza Kufungwa kwa Imani Yao Katika Eneo la Kursk

HABARI ZA KARIBUNI | Wenzi wa Ndoa na Ndugu Watatu Wahukumiwa Nchini Urusi

Juni 3, 2021, Mahakama ya Wilaya ya Viwanda iliyoko Kursk iliwahukumu wenzi wa ndoa na ndugu wengine watatu. Ndugu Andrey Andreyev alihukumiwa kifungo cha miaka minne na nusu gerezani na Ndugu Andrey Ryshkov akahukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani. Ndugu Artem Bagratyan alihukumiwa kifungo cha miaka miwili na nusu gerezani na mke wake, Alevtina, akahukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani. Ndugu Aleksandr Vospitanyuk, ambaye aliongezwa kwenye kesi hiyo, alihukumiwa miaka miwili chini ya usimamizi wenye masharti.

Hukumu Inatarajiwa

Mahakama ya Viwanda ya Wilaya katika eneo la Kursk itasikiliza kesi dhidi ya Ndugu Andrey Andreyev, Ndugu Artem Bagratyan na mke wake, Alevtina, na Ndugu Andrey Ryshkov. a

Maelezo Mafupi Kumhusu

Andrey Andreyev

  • Alizaliwa: 1976 (Kursk)

  • Maisha Yake: Alifunga ndoa na Svetlana mnamo 1999. Ana binti wawili. Alianza kupendezwa na Biblia alipojifunza kuhusu kutimia kwa unabii wa Biblia. Alibatizwa mnamo 2002

Alevtina Bagratyan

  • Alizaliwa: 1977 (Kursk)

  • Maisha Yake: Alifurahia sanaa alipokuwa mtoto. Alianza kujifunza Biblia alipokuwa na umri mdogo sana. Alibatizwa katika mwaka 1997. Alifunga ndoa na Artem mnamo 2012. Amefanya kazi akiwa msusi huku akimtunza pia mama yake

Artem Bagratyan

  • Alizaliwa: 1972 (Abovyan, Armenia)

  • Maisha Yake: Alihamia Armenia kutoka Urusi. Alikutana na Alevtina huko Kursk. Wote wawili wanapenda kuchunguza vitu vya asili. Alibatizwa mnamo 2000

Andrey Ryshkov

  • Alizaliwa: 1987 (Kursk)

  • Maisha Yake: Baba yake alikufa alipokuwa mvulana. Alipokuwa kijana aliishi muda mrefu pamoja na babu yake huku mama yake akiwa ameajiriwa kufanya kazi mbili. Alipendezwa na Biblia baada ya kupata majibu ya maswali yaliyomhangaisha kwa miaka mingi. Alibatizwa mnamo 2011. Alifunga ndoa na Marina katika mwaka wa 2016. Amefanya kazi ya kukarabati nyumba za makazi

Historia ya Kesi

Oktoba 16, 2019, maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa (FSB) walifanya upekuzi mkubwa na kuwahoji Mashahidi wa Yehova katika eneo la Kursk. Baada ya hapo Ndugu Andrey Andreyev pamoja na Ndugu na Dada Bagratyan walikamatwa. Kisha Ndugu Ryshkov alikamatwa Januari 21, 2020. Alevtina Bagratyan aliachiliwa Desemba 17, 2020, baada ya kukaa mahabusu kwa miezi 13. Sasa yuko katika kifungo cha nyumbani. Ndugu hao watatu bado wako mahabusu.

Artem Bagratyan anaugua ugonjwa wa kisukari. Alevtina anakumbuka wakati ambapo yeye na mume wake walifungwa katika jela tofauti. Anasema hivi: “Kwa muda mrefu, ilikuwa vigumu kujua anaendeleaje, ikiwa afya yake ilikuwa ikizorota. Nilimkosa sana.”

Alevtina anasema kwamba aliendelea kuwa na uhakika kwamba Yehova atamtunza pamoja na ndugu hao muda wote ambapo wangefungwa. Anaeleza hivi: “Sikuzote [Yehova] ameniimarisha. Ninajua kwamba ataendelea kufanya hivyo. Sina shaka naye.”

Tuna uhakika kwamba Yehova ataendelea kuwa mnara wenye nguvu kwa ndugu zetu watatu na Dada Alevtina kesi yao inapoendelea.—Methali 18:10.

a Tarehe ya hukumu haitolewi mapema pindi zote.