Hamia kwenye habari

Ndugu Anatoliy Isakov na mke wake, Tatyana

JANUARI 1, 2024
URUSI

‘Yehova Ameshikamana Nami’

‘Yehova Ameshikamana Nami’

Mahakama ya Jiji la Kurgan iliyo katika Eneo la Kurgan itatangaza hivi karibuni uamuzi wake katika kesi inayomhusu Ndugu Anatoliy Isakov. Mwendesha-mashtaka bado hajatoa ombi la hukumu anayopendekeza.

Maelezo Mafupi Kumhusu

Tunatiwa moyo na mfano wa Anatoliy kwa sababu yeye ni mtu thabiti na ameonyesha imani licha ya changamoto anazokabili. Nasi tunafarijika kujua kwamba katika changamoto zote tunazokabili, Yehova atakuwa ‘mwamba wa mioyo’ yetu.​—Zaburi 73:26.

Mfuatano wa Matukio

  1. Julai 13, 2021

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa

  2. Julai 14, 2021

    Nyumba yake ilifanyiwa msako. Aliwekwa kizuizini

  3. Julai 15, 2021

    Alihamishiwa mahabusu

  4. Julai 21, 2021

    Rufaa ilikatwa katika Idara ya Afya ya Eneo la Kurgan kuomba Anatoliy aachiliwe ili aweze kuendelea na matibabu ya kemikali

  5. Agosti 28, 2021

    Aliachiliwa kutoka mahabusu baada ya Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu kutuma ombi. Amewekewa vizuizi vya kusafiri

  6. Julai 6, 2023

    Kesi ya uhalifu ilianza