Hamia kwenye habari

Ndugu Yevgeniy Korotun

NOVEMBA 25, 2021
URUSI

Yehova Amfariji Ndugu Yevgeniy Korotun

Yehova Amfariji Ndugu Yevgeniy Korotun

Mfuatano wa Matukio

  1. Mahakama ya Jiji la Severskiy iliyo katika Eneo la Tomsk itatangaza hivi karibuni hukumu yake katika kesi ya Ndugu Yevgeniy Korotun. a Mwendesha-mashtaka bado hajatoa ombi la hukumu anayopendekeza

  2. Machi 31, 2021

    Kesi ilianza

  3. Septemba 7, 2020

    Aliwekwa kizuizini na kisha akahamishiwa mahabusu baada ya kupelekwa mahakamani

  4. Julai 15, 2020

    Aliwekwa kwenye kifungo cha nyumbani

  5. Julai 14, 2020

    Maofisa wa FSB walifanya msako katika nyumba za familia nne za Mashahidi wa Yehova huko Seversk, kutia ndani nyumba ya familia ya Korotun

  6. Julai 13, 2020

    Kesi ya uhalifu dhidi ya Yevgeniy ilifunguliwa

  7. 2018-2019

    Wapelelezi wawili walijifanya kupendezwa na mazungumzo ya Biblia na wakarekodi kisiri mazungumzo yao ili wayatumie kama ushahidi dhidi ya Yevgeniy

Maelezo Mafupi Kumhusu

Tuna uhakika kwamba Yehova anategemeza familia ya Korotun na wote wanaomtumikia kwa uaminifu licha ya hali ngumu.—Waroma 15:5.

a Tarehe ya hukumu haitolewi mapema pindi zote.

b Kwa sababu Ndugu Korotun yuko mahabusu kwa sasa, haikuwezekana kuzungumza naye ili kujua maoni yake.