Hamia kwenye habari

Kushoto hadi kulia: Ndugu Aleksandr Sobyanin, Ndugu Vladimir Timoshkin, na Ndugu Vladimir Poltoradnev

SEPTEMBA 12, 2023
URUSI

“Yehova Hutupa Msaada Sikuzote!”

“Yehova Hutupa Msaada Sikuzote!”

Agosti 18, 2023, Mahakama ya Jiji la Solikamsk iliyo katika Eneo la Perm iliwahukumu Ndugu Vladimir Poltoradnev, Ndugu Aleksandr Sobyanin, na Ndugu Vladimir Timoshkin. Walitozwa faini ya rubo 638,000 (dola 6,787 za Marekani), rubo 494,000 (dola 5,255 za Marekani), na rubo 512,000 (dola 5,447 za Marekani) mtawalia. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tuna uhakika kwamba wote wanaomtumaini Yehova watanufaika na upendo wake mshikamanifu.​—Zaburi 13:5, 6.

Mfululizo wa Matukio

  1. Julai 28, 2020

    Nyumba zilifanyiwa msako. Ndugu hao watatu waliwekwa kizuizini

  2. Julai 29, 2020

    Vladimir Timoshkin alitolewa kizuizini na kuwekwa kwenye kifungo cha nyumbani

  3. Julai 30, 2020

    Aleksandr alitolewa kizuizini na kuwekewa vizuizi vya kusafiri

  4. Julai 31, 2020

    Vladimir Poltoradnev alitolewa kizuizini na kuwekwa kwenye kifungo cha nyumbani

  5. Septemba 24, 2020

    Vladimir Poltoradnev alitolewa kwenye kifungo cha nyumbani na kuwekewa vizuizi vya kusafiri

  6. Oktoba 26, 2020

    Vladimir Timoshkin alitolewa kwenye kifungo cha nyumbani na kuwekewa vizuizi vya kusafiri

  7. Mei 16, 2023

    Kesi ya uhalifu ilianza

a Hatukuweza kupata maelezo ya Ndugu Vladimir Timoshkin.