Hamia kwenye habari

JULAI 14, 2016
URUSI

Mahakama Itasikiliza Rufani ya Mashahidi Dhidi ya Vitisho vya Kufunga Makao Makuu Nchini Urusi

Mahakama Itasikiliza Rufani ya Mashahidi Dhidi ya Vitisho vya Kufunga Makao Makuu Nchini Urusi

Mahakama ya Wilaya ya Tver ya Moscow ilikubali kusikiliza rufani ya Mashahidi kupinga barua ya onyo kutoka kwa Mwendesha-Mashtaka Mkuu iliyotishia kufunga makao yao makuu nchini Urusi. Mahakama itasikiliza kesi hiyo Julai 18, 2016 ili kuamua ikiwa inakubalika kisheria kutoa onyo hilo.

Makaimu katika Baraza la Mkoa la Arkhangelsk walifungua kesi nyingine dhidi ya Mashahidi wa Yehova nchini Urusi. Walifikisha kesi hiyo kwa Waziri wa Sheria, Aleksandr Konovalov. Kusudi la kuwasilisha kesi yao ni kwamba serikali ya Urusi ipitishe sheria ya kupiga marufuku utendaji wa kidini wa Mashahidi na mashirika yao ya kisheria nchini kote.