OKTOBA 31, 2013
URUSI
Baraza Kuu la Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu Lakataa Kuchunguza Upya Kesi Dhidi ya Urusi
Jumatatu, Oktoba 7, 2013, Baraza Kuu la Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu lilikataa ombi la nchi ya Urusi la kuchunguza upya uamuzi ambao Mahakama hiyo ya Ulaya ilifikia mnamo Juni 6 kuhusiana na kesi inayowahusu Mashahidi wa Yehova. Nchi ya Urusi ilipatikana na hatia ya kukiuka haki ya msingi ya kuwa na faragha na ikaagizwa na Mahakama ya Ulaya iwalipe fidia Bi. V. Zhukova na Bi. Y. Avilkina. Kila mmoja wao alipaswa kulipwa fidia ya euro 5,000 (au dola 6,622). Maofisa wa serikali ya Urusi walikuwa wamechukua kutoka hospitalini rekodi za kibinafsi za kitiba za wanawake hao bila idhini. Serikali ya Urusi iliomba kesi hiyo ipelekwe kwenye Baraza Kuu la Mahakama hiyo ambalo lina mamlaka ya kuichunguza upya. Hata hivyo Mahakama hiyo ilikataa ombi la serikali ya Urusi. Uamuzi huo uliofikiwa Juni 6 ulikuwa ndio wa kukata maneno, na kwa hiyo basi Serikali ya Urusi iko chini ya wajibu wa kuheshimu haki ya msingi ya faragha katika hali kama hizo na pia inapaswa kuwalipa wanawake hao fidia kulingana na amri ya Mahakama hiyo.
Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:
J. R. Brown, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1 718 560 5000
Urusi: Grigory Martynov, simu +7 812 702 2691