AGOSTI 22, 2018
URUSI
Kutoka Gerezani Hadi Kifungo cha Nyumbani
Agosti 3, 2018, Hakimu Inna Yangubayeva wa Mahakama ya Wilaya ya Leninsky iliyoko Orenburg, Urusi, aliwahukumu Ndugu Vladimir Kochnev na Aleksandr Suvorov kifungo cha nyumbani baada ya kila mmoja wao kufungwa gerezani kwa siku 78. Siku hiyohiyo katika Mahakama ya Eneo la Magadan, Ndugu Konstantin Petrov pia alihukumiwa kifungo cha nyumbani baada ya kuwa gerezani kwa siku 64. Ingawa tunashukuru kwamba ndugu zetu watatu hawapo gerezani sasa, bado wanasubiri kesi zao, na wakipatikana kuwa wana hatia wanaweza kupata kifungo cha hadi miaka kumi gerezani.
Kufikia Agosti 16, kulikuwa na Mashahidi 9 waliohukumiwa kifungo cha nyumbani na 25 wako gerezani kotekote nchini Urusi. Ndugu na dada wengine 30 wamelazimishwa kutia sahihi hati inayowakataza kutoka kwenye miji yao bila ruhusa ya wenye mamlaka. Tunaendelea kusali kwa ajili ya ndugu na dada zetu ambao wanakabili hali ngumu sana nchini Urusi.—2 Wakorintho 1:11.