Hamia kwenye habari

JULAI 22, 2016
URUSI

Kesi ya Tishio la Kufungwa kwa Makao Makuu ya Mashahidi Nchini Urusi Imeahirishwa Mpaka Septemba

Kesi ya Tishio la Kufungwa kwa Makao Makuu ya Mashahidi Nchini Urusi Imeahirishwa Mpaka Septemba

Mahakama ya Wilaya ya Tver jijini Moscow imesikiliza kesi ya rufaa ya Mashahidi kupinga barua ya onyo ya Mwendesha Mashtaka Mkuu iliyotishia kufungwa kwa makao yao makuu ya nchi hiyo. Mahakama ilisikiliza maelezo ya awali na kuahirisha kesi hiyo mpaka Septemba 23, 2016. Wakati huo mahakama hiyo itaendesha kesi hiyo yote. Mabalozi wa nchi mbalimbali waliopo Moscow watahudhuria.

Matukio ya karibuni ya serikali yanatishia uhuru wa ibada ya Mashahidi. Marekebisho mapya ya sheria ya Urusi kuhusiana na Uhuru wa Dhamiri na Mashirika ya Dini yataanza kufanya kazi Julai 20, 2016. Baada ya muda tutaona wazi jinsi wenye mamlaka nchini Urusi watatumia sheria hizo mpya kuelekea utendaji wa Mashahidi wa Yehova.