APRILI 5, 2017
URUSI
Mahakama Kuu Inaendelea Kusikiliza Kesi ya Kuwapiga Marufuku Mashahidi wa Yehova Nchini Urusi
Mahakama Kuu ya Urusi ilitangaza mapumziko leo baada ya kusikiliza taarifa mbalimbali katika kesi ya kuwapiga marufuku Mashahidi wa Yehova. Wizara ya Haki iliwasilisha shtaka linalotaka “shirika la kidini, yaani, Kituo cha Usimamizi cha Mashahidi wa Yehova, kitangazwe kuwa na msimamo mkali wa kidini, utendaji wake upigwe marufuku, na kituo hicho kifungwe.” Mahakama itaendelea kusikiliza kesi hiyo Aprili 6, 2017, saa 8:00 alasiri.
Mark Sanderson, mshiriki wa Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova, aliyekuwepo wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, alisema hivi: Inasikitisha kwamba Mahakama Kuu ilipuuza au kukataa maombi mengi yaliyotolewa na Kituo cha Usimamizi. Wawakilishi wa ubalozi mbalimbali na mashirika ya haki za kibinadamu walikuwepo wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo. Dunia nzima inatazama.”