Hamia kwenye habari

APRILI 12, 2017
URUSI

Mahakama Kuu Yasikiliza Ushahidi wa Mashahidi wa Yehova Dhidi ya Marufuku

Mahakama Kuu Yasikiliza Ushahidi wa Mashahidi wa Yehova Dhidi ya Marufuku

Aprili 12 2017, Mahakama Kuu iliendelea kwa siku ya nne kusikiliza kesi ya kuwapiga marufuku Mashahidi wa Yehova nchini Urusi. Mawakili wa Kituo cha Usimamizi cha Mashahidi walionyesha kwa nini dai lililotolewa na Wizara ya Haki linakiuka mikataba ya kimataifa ya Urusi na katiba ya nchi hiyo.

Mawakili hao walionyesha kwamba marufuku iliyopendekezwa na Wizara ya Haki inakiuka sheria za kimataifa, kutia ndani Mkataba wa Ulaya na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa. Mikataba hiyo, pamoja na katiba ya Urusi, inahakikisha kwamba uhuru wa dhamiri na dini, uhuru wa kusema, uhuru wa kukutana, na uhuru wa kuwa na mashirika (haki ya kufanyiza mashirika ya kisheria).

Mashahidi wanne wa Yehova walitoa ushahidi kwamba makutaniko yao hayatumii machapisho yaliyo katika Orodha ya Serikali ya Vitabu na Habari Zinazowachochea Watu Kuwa na Msimamo Mkali wa Kidini (FLEM) na kwamba Mashahidi hawawezi kuhusianishwa na msimamo mkali. Mahakama ilitangaza mapumziko na itaendelea kusikiliza kesi Aprili 19, 2017, saa 4:00 asubuhi.