Hamia kwenye habari

APRILI 7, 2017
URUSI

Kesi ya Kuwapiga Marufuku Mashahidi wa Yehova Inaendelea Kusikilizwa kwa Siku ya Tatu

Kesi ya Kuwapiga Marufuku Mashahidi wa Yehova Inaendelea Kusikilizwa kwa Siku ya Tatu

Kwa siku ya tatu Mahakama Kuu ya Shirikisho la Urusi imeendelea kusikiliza kesi ya kutaka kuwapiga marufuku Mashahidi wa Yehova nchini Urusi. Kati ya wale waliotoa ushahidi, kulikuwa na wasimamizi wawili wa Kituo cha Usimamizi ambao walitoa ushahidi kupinga dai la Wizara ya Haki dhidi ya Mashahidi wa Yehova.

Sergey Cherepanov alipinga agizo la Wizara ya Haki kwamba Kituo cha Usimamizi kinapaswa kuacha kuvunja sheria kuhusu msimamo mkali. Hata hivyo, Wizara ya Haki haikufafanua jinsi Kituo cha Usimamizi kilivyokiuka sheria hiyo au jinsi ambavyo kingeacha kuivunja. Msimamizi mwingine, Vasiliy Kalin, alisema kwamba Kituo cha Usimamizi kimekuwa kikitenda kwa miaka 26, kisha akauliza: “Ni lini hasa tulipoanza kuwa na msimamo mkali?” Aliongezea kwamba Mashahidi wa Yehova hawajabadilika kwa njia yoyote—bado wanatii mamlaka na sikuzote wanashikamana na kanuni za amani. Alisema inasikitisha kwamba tayari Mashahidi wameanza kuteswa nchini.

Hakimu alisema kesi itaendelea Aprili 12, 2017, saa 4:00 asubuhi.