Hamia kwenye habari

NOVEMBA 11, 2014
URUSI

Kesi Kuhusu Kufungwa kwa Shirika la Kisheria la Mashahidi Jijini Samara Itaendelea

Kesi Kuhusu Kufungwa kwa Shirika la Kisheria la Mashahidi Jijini Samara Itaendelea

Novemba 12, 2014 ndiyo tarehe iliyopangwa na Mahakama Kuu ya Shirikisho la Urusi kuendelea kusikiliza kesi inayohusu jaribio la kufunga shirika la kisheria la Mashahidi wa Yehova jijini Samara. Kesi hiyo ilianza Oktoba 8, zaidi ya mwezi mmoja uliopita, na wanahabari, watazamaji kutoka ofisi za ubalozi, mawakili, na Mashahidi wenzao walijaa katika chumba kikubwa cha Mahakama hiyo. Baada ya kufanya mambo fulani ya utangulizi, Mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi wakati mwingine.

Vasily Kalin, mwakilishi wa Kituo cha Usimamizi cha Mashahidi wa Yehova nchini Urusi, alisema hivi: “Tunatumaini kwamba Mahakama Kuu inayoheshimika nchini Urusi itatekeleza haki katika kesi hii na kufuata viwango vya katiba ya jamii ya kidemokrasia kwa kutupilia mbali madai yanayotolewa na mwendesha-mashtaka.” Mashahidi wa Yehova wanatumaini kwamba Mahakama hiyo itatetea haki yao ya uhuru wa ibada kama ilivyoonyeshwa katika Katiba ya Urusi.