Hamia kwenye habari

APRILI 5, 2017
URUSI

Mahakama Kuu ya Urusi Yaanza Kesi Kubwa Dhidi ya Mashahidi wa Yehova

Mahakama Kuu ya Urusi Yaanza Kesi Kubwa Dhidi ya Mashahidi wa Yehova

NEW YORK—Leo, Mahakama Kuu ya Shirikisho la Urusi ilianza kusikiliza kesi ya Wizara ya Haki kwamba Kituo cha Usimamizi cha Mashahidi wa Yehova nchini Urusi kifungwe. Mahakama hiyo ilitangaza mapumziko na kwamba kesi itaendelea kusikilizwa Alhamisi Aprili 6, 2017, saa 8:00 alasiri.

Mashahidi walifikisha mashtaka kwenye Mahakama hiyo mnamo Machi 30, 2017, dhidi ya Wizara ya Haki. Hata hivyo, leo mashtaka hayo yalitupiliwa mbali na Mahakama hiyo kabla ya mapumziko. Pia, Mahakama hiyo ilikataa kuwaruhusu wataalamu watoe ushahidi kuhusu msingi wa dai la Wizara ya Haki na ikakataa kuwaruhusu wale walioshuhudia kupandikizwa kwa ushahidi dhidi ya mashirika ya kidini ya Mashahidi wa Yehova.

Kwa kuwa kesi hiyo ni kubwa sana, vyombo vya habari vya kimataifa vinaikazia fikira. Kwa mfano, makala moja kwenye gazeti Time iliwekwa kwenye mtandao mnamo Aprili 4 (“Mahakama Kuu ya Urusi Inafikiria Kupiga Marufuku Ibada ya Mashahidi wa Yehova”) na makala ya Aprili 5 kwenye ukurasa wa kwanza katika gazeti lililochapishwa la The New York Times (“Wakristo, Wasiounga Mkono Vita Wanatishwa Kupigwa Marufuku na Urusi Eti Wana Msimamo Mkali”).

David A. Semonian, msemaji wa Mashahidi kwenye makao yao makuu ya ulimwenguni pote kule New York anasema hivi: “Tunatumaini kwamba Mahakama Kuu ya Urusi itatetea haki za waamini wenzetu nchini Urusi za kuabudu kwa amani na kwa uhuru. Mamilioni ya watu ulimwenguni pote watakuwa wakitazama kwa makini kuona jinsi kesi hiyo inavyoendelea na ikiwa Urusi itatenda ili kuwalinda raia wake wanaotii sheria ambao ni Mashahidi wa Yehova.”

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000

Urusi: Yaroslav Sivulskiy, +7-812-702-2691