Hamia kwenye habari

APRILI 6, 2017
URUSI

Mahakama Kuu ya Urusi Inaendelea Kusikiliza Kesi Dhidi ya Mashahidi wa Yehova

Mahakama Kuu ya Urusi Inaendelea Kusikiliza Kesi Dhidi ya Mashahidi wa Yehova

Katika siku ya pili ya kesi hii, Mahakama Kuu ya Shirikisho la Urusi iliendelea kusikiliza dai la Wizara ya Haki la kutaka Kituo cha Usimamizi cha Mashahidi wa Yehova nchini Urusi kifungwe. Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Ijumaa, Aprili 7, 2017, saa 4:00 asubuhi.

David A. Semonian, msemaji wa Mashahidi katika makao makuu ya ulimwenguni pote yaliyoko New York, anaeleza hivi: “Leo matukio mahakamani yalifunua kwamba Wizara ya Haki haina msingi wa madai yao dhidi ya tengenezo letu.” Aliongezea hivi, “Lakini pia Wizara ya Haki ilisema waziwazi kwamba ikiwa Mashahidi wa Yehova wanapigwa marufuku, wanaweza kuhukumiwa kama wahalifu ikiwa tu watakutana kutoa sala. Tunatumaini kwamba Mahakama Kuu itatetea haki na kuzuia kukiukwa kwa haki zetu za msingi za kibinadamu.”

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000

Urusi: Yaroslav Sivulskiy, +7-812-702-2691