OKTOBA 4, 2017
URUSI
Mahakama ya Rufaa Imeamua Dennis Christensen Aendelee Kubaki Mahabusu
Septemba 28, 2017, baada ya kusikiliza kesi kwa saa tatu, Mahakama ya Mkoa wa Oryol ilikataa kutoa rufaa ya kumwachilia Dennis Christensen, raia wa Denmark ambaye ni Shahidi wa Yehova. Ataendelea kuwa mahabusu hadi Novemba 23, 2017.
Wakati kesi ya Bw. Christensen ilipokuwa ikisikilizwa mnamo Julai, mahakama ya chini iliongeza isivyo haki muda wa kukaa mahabusu hadi Novemba, ili kumruhusu mwendesha mashtaka apate “uthibitisho” wa mashtaka ya kuwa na msimamo mkali wa kidini. Wakili wa Bw. Christensen walifungua kesi kwenye Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu (ECHR), na Septemba 4, 2017, ECHR ilianza uchunguzi wa kesi hiyo kwa kuiuliza serikali ya Urusi maswali mengi kuhusu kukiuka haki za Bw. Christensen.
Kesi ya Bw. Christensen inaangaziwa kimataifa kwa sababu ndio kesi pekee tangu enzi za Sovieti inayohusu nchi ya Urusi kumfunga Shahidi kwa sababu tu ya kushiriki ibada.