Hamia kwenye habari

DESEMBA 27, 2018
URUSI

Mahakama ya Urusi Yamhukumu Arkadya Akopyan Mwenye Umri wa Miaka 70

Mahakama ya Urusi Yamhukumu Arkadya Akopyan Mwenye Umri wa Miaka 70

Hakimu Oleg Golovashko wa Mahakama ya Wilaya ya Prohladniy ametoa hukumu katika kesi dhidi ya Ndugu Arkadya Akopyan Alhamisi, Desemba 27. Mahakama ilimhukumu Ndugu Akopyan, mwenye umri wa miaka 70, ambaye ni fundi-nguo aliyestaafu, afanye huduma kwa jamii kwa saa 120 kwa madai yasiyo na msingi kwamba aliwalipa watu wasio Mashahidi wasambaze machapisho yenye msimamo mkali.

Ingawa Ndugu Akopyan hakufungwa gerezani, hukumu hiyo inapingana kabisa na haki za kibinadamu. Hivyo, atakata rufaa katika mahakama ya juu.

Katika majuma yajayo, tunatarajia kwamba hukumu itatolewa katika kesi inayomhusu Dennis Christensen. Tunasali kwamba Yehova aendelee kuwategemeza na kuwafariji ndugu na dada zetu nchini Urusi wanaokabili vifungo kwa sababu ya imani yao.—2 Wathesalonike 2:16, 17.