APRILI 7, 2017
URUSI
Siku ya Tatu ya Kesi Katika Mahakama Kuu ya Urusi, Mashahidi wa Yehova Watoa Ushahidi
NEW YORK—Siku ya tatu ya kusikilizwa kwa kesi mbele ya Mahakama Kuu ya Urusi imekwisha, na Mahakama imetangaza mapumziko hadi Jumatano, Aprili 12, 2017, saa 4:00 asubuhi. Leo, Mahakama ilisikiliza ushahidi kutoka kwa Mashahidi wanne wa Yehova, ambao walitoa ushahidi dhidi ya dai la Wizara ya Haki la kufunga Kituo cha Usimamizi cha Mashahidi wa Yehova na kupiga marufuku utendaji wao.
Hakimu aliuliza Wizara ya Haki maswali kadhaa, akiwaomba watoe ushahidi unaounga mkono mashtaka yao kwamba Mashahidi wa Yehova wana msimamo mkali na kwamba wanasambaza machapisho yenye msimamo mkali. Wizara ya Haki haikuweza kufanya hivyo. Vasiliy Kalin, mshiriki wa halmashauri inayosimamia Kituo cha Usimamizi cha Mashahidi wa Yehova nchini Urusi, alisema hivi alipokuwa mbele ya Mahakama: “Ningependa kuikumbusha Wizara ya Haki kwamba ombi lao la kuwapiga marufuku Mashahidi wa Yehova litawaumiza watu ambao wanawatakia ninyi maisha yenye amani na furaha.”
Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:
David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000
Urusi: Yaroslav Sivulskiy, +7-911-087-8009