Matukio Muhimu Kihistoria Nchini Urusi
MEI 5, 2018—Mahakama ya Jiji la St Petersburg City iliunga mkono uamuzi wa serikali wa kutaifisha Kituo cha Usimamizi cha Mashahidi wa Yehova
JULAI 17, 2017—Mahakama Kuu ya Rufaa ya Shirikisho la Urusi iliunga mkono uamuzi wa mahakama wa Aprili 20. Ibada ya Mashahidi wa Yehova ikapigwa marufuku katika nchi nzima
APRILI 20, 2017—Mahakama Kuu ya Shirikisho la Urusi ilitoa uamuzi wa kufanya utendaji wa Mashahidi wa Yehova uwe kosa la jinai nchini Urusi
NOVEMBA 30, 2015—Mashahidi wote kumi na sita ambao kesi yao ilisikilizwa upya katika jiji la Taganrog walihukumiwa kuwa na hatia kwa sababu ya imani yao. Hakimu aliahirisha hukumu zao za gerezani
DESEMBA 2, 2014—Mahakama Kuu ya Shirikisho la Urusi ilipiga marufuku jw.org
JULAI 30, 2014—Mashahidi saba kati ya Mashahidi kumi na sita walihukumiwa na mahakama ya Taganrog kuwa wahalifu kwa sababu ya imani yao
JUNI 10, 2010—Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu ilitangaza kwamba Mashahidi wa Yehova wa Moscow wamepigwa marufuku kinyume cha haki za kibinadamu
SEPTEMBA 11, 2009—Mahakama ya Mkoa wa Rostov ilitangaza kwamba machapisho 34 yanayochapishwa na Mashahidi wa Yehova kuwa yenye msimamo mkali
2009—Maofisa wa polisi walianza kutumia vibaya Sheria ya Shirikisho la Kupambana na Shughuli Zenye Msimamo Mkali
MACHI 26, 2004—Mashahidi wa Yehova wa Moscow walipigwa marufuku
MACHI 1996—Tangazo latolewa kwamba Mashahidi wa Yehova wamekuwa wakikandamizwa isivyo haki kwa sababu za kisiasa
DESEMBA 11, 1992—Shirikisho la Urusi lilisajili Mashahidi wa Yehova kisheria
MACHI 27, 1991—Muungano wa Sovieti ilisajili Mashahidi wa Yehova kisheria
OKTOBA 1965—Vizuizi viliyowekwa na serikali vilianza kupunguzwa na pia ukandamizaji ulianza kupungua
APRILI 1951—Mashahidi 9,500 hivi kutoka katika jamhuri mbalimbali za Sovieti walipelekwa uhamishoni Siberia
1928—Mashahidi wa Yehova hawakufaulu kupata usajili wa kisheria; mwanzo wa miaka mingi ya mateso
1891—Shahidi wa kwanza Mrusi alipelekwa uhamishoni Siberia
1887—Rekodi ya gazeti la kwanza la Mnara wa Mlinzi kutumwa nchini Urusi