Hamia kwenye habari

JUNI 15, 2018
URUSI

Urusi Yataifisha Ofisi ya Tawi

Urusi Yataifisha Ofisi ya Tawi

Mei 3, 2018, Mahakama ya Jiji la Saint Petersburg imeunga mkono uamuzi wa Desemba 2017, na hivyo kuiruhusu serikali ya Urusi kuchukua mara moja ofisi yetu ya tawi iliyoko Solnechnoye. Muda mfupi kabla ya kusikilizwa kwa rufaa hiyo, mwandishi wa habari, mtaalamu wa kidini, na mawakili wawili Mashahidi walifunua kwamba huo ni ukosefu wa haki katika sheria. Wenzi wa ndoa ambao walisaidia ujenzi wa ofisi hiyo wanaeleza thamani ya ofisi hiyo kwao.