Hamia kwenye habari

APRILI 17, 2018
URUSI

Mahakama Itasikiliza Rufaa Inayopinga Serikali ya Urusi Kuchukua Ofisi ya Taifa ya Mashahidi

Mahakama Itasikiliza Rufaa Inayopinga Serikali ya Urusi Kuchukua Ofisi ya Taifa ya Mashahidi

Mei 3, 2018, Mahakama ya Jiji la St Petersburg itasikiliza rufaa ya Mashahidi wa Yehova kupinga hukumu ya awali ya mahakama iliyodai kwamba ofisi yao ya zamani ya taifa nchini Urusi itaifishwe. Ikiwa Mashahidi hawatashinda kwenye rufaa hiyo, uamuzi huo utatekelezwa haraka na Serikali inaweza kuyachukua majengo hayo.

Awali Mahakama ya Wilaya ya Sestroretskiy ilikataa uthibitisho unaoonyesha kwamba ofisi hiyo ya Mashahidi inamilikiwa na Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania (WTPA), shirika la kimataifa lisilo la kibiashara ambalo limeandikishwa nchini Marekani. WTPA imemiliki na kuyalipia kodi majengo hayo kwa miaka 17. Hata hivyo, Desemba 7, 2017, mahakama ya wilaya ilitangaza kwamba mkataba wa umiliki wa WTPA hautambuliki kisheria. Ikiwa Mashahidi watashindwa wakati rufaa hiyo itakaposikilizwa na wasipopata msaada wa kisheria katika mahakama nyingine za Urusi, watapeleka kesi hiyo katika Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu ili ishughulikie ukosefu huo mkubwa wa haki.

Kesi itaanza kusikilizwa saa 05:30 asubuhi, Mei 3, 2018, katika Mahakama ya Jiji la St Petersburg, ul. Basseynaya, 6, St. Petersburg, Urusi.