Hamia kwenye habari

MEI 1, 2018
URUSI

Wenye Mamlaka Nchini Urusi Wajaribu Kunyakua Mali Inayomilikiwa na Shirika la Mashahidi wa Yehova la Marekani

Wenye Mamlaka Nchini Urusi Wajaribu Kunyakua Mali Inayomilikiwa na Shirika la Mashahidi wa Yehova la Marekani

NEW YORK—Alhamisi, Mei 3, 2018, Mahakama ya Jiji la Saint Petersburg itasikiliza rufaa ya Mashahidi wa Yehova kuhusu hukumu iliyotolewa ya kunyakua ofisi yao ya kitaifa nchini Urusi. Rufaa yao ikikataliwa, Serikali inaweza kunyakua eneo hilo lenye majengo 14 mara moja. Mali hiyo iliyo kwenye eneo la ekari 25 inakadiriwa kuwa na thamani ya dola milioni 31.8 (rubo bilioni 2).

Hukumu ya kwanza iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya ya Sestroretskiy Desemba 2017 ilipuuza uthibitisho kwamba ofisi ya Mashahidi inamilikiwa na Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania (WTPA), shirika lisilo la kibiashara nchini Marekani. Mashahidi wa Yehova nchini Urusi walihamisha umiliki wa ofisi hiyo kwa WTPA mwaka wa 2000, na WTPA imelipa dola milioni 3 (rubo milioni 188) ya kodi kwa Serikali ya Urusi. Ingawa serikali ya Urusi ilitambua badiliko hilo la kisheria la umiliki kwa miaka zaidi ya 17, mahakama ya wilaya sasa inasema kwamba mkataba wa umiliki wa WTPA hautambuliki kisheria. Kwa sababu hiyo, mahakama imetangaza Kituo cha Usimamizi cha Mashahidi nchini Urusi kuwa mmiliki. Kwa kuwa Kituo cha Usimamizi kilipigwa marufuku na Mahakama Kuu mwaka wa 2017, rufaa ya Mashahidi ikikataliwa, uamuzi huo utatekelezwa, na Serikali inaweza kunyakua mali hiyo mara moja.

Kesi itasikilizwa saa 5:30 asubuhi katika Mahakama ya Jiji la Saint Petersburg City Court, ul. Basseynaya, 6, St. Petersburg, Urusi.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000