MEI 3, 2018
URUSI
Rufaa ya Mashahidi Imekataliwa, Mamlaka Nchini Urusi Zinaweza Kunyakua Ofisi ya Tawi
Alhamisi, Mei 3, 2018, Mahakama ya Jiji la Saint Petersburg imeunga mkono uamuzi uliotolewa Desemba 2017, na kuiruhusu serikali ya Urusi inyakue mara moja ofisi yetu ya tawi nchini Urusi iliyoko Solnechnoye.
Ingawa hatuwezi kuizuia nchi ya Urusi kunyakua mali yetu, hukumu hiyo ni sehemu ya maombi yanayoshughulikiwa na Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu (ECHR). Mahakama hiyo imeiambia serikali ya Urusi kwamba maombi yetu yatashughulikiwa haraka.
Tunaendelea kumtegemea Yehova, Mungu wa haki kamili, kusuluhisha jambo hilo kwa wakati unaofaa.—Isaya 30:18.