OKTOBA 26, 2016
URUSI
Mahakama Kuu ya Shirikisho la Urusi Yaongeza Vizuizi Dhidi ya Ibada ya Mashahidi wa Yehova
Oktoba 18, 2016, Mahakama Kuu ya Shirikisho la Urusi iliunga mkono uamuzi wa mahakama ya chini wa kufungwa kwa shirika la kisheria la Mashahidi wa Yehova jijini Orel kwa madai kwamba lina “msimamo mkali.” Hili ni shirika la saba ambalo limefungwa na mahakama za Urusi. Mashirika hayo yote ya kisheria yamefungwa kwa sababu ya kutumiwa vibaya kwa sheria ya msimamo mkali dhidi ya ibada ya Mashahidi wa Yehova.
Hapo awali wenye mamlaka jijini Orel walikuwa wamejaribu kulifunga shirika la kisheria la Mashahidi jijini Orel kwa madai ya uwongo. Waliposhindwa kufanya hivyo, Wizara ya Haki ilifungua kesi mnamo Mei 2016, ikidai kwamba shirika la kisheria la Orel ni shirika lenye “msimamo mkali.”
Kesi hiyo kuhusu shirika la kisheria la Orel ni muhimu sana kwa sababu shirika hilo ndilo la kwanza kupokea onyo na kufungwa tangu Ofisi ya Mwendesha-Mashtaka Mkuu itoe onyo dhidi ya ofisi ya kitaifa ya Mashahidi nchini Urusi mnamo Machi 2016.