JULAI 16, 2014
URUSI
Mahakama ya Urusi Itatangaza Uamuzi Wake: Mashahidi wa Yehova Wameshtakiwa Kuwa Wahalifu kwa Sababu ya Imani Yao
Julai 28, 2014, Mahakama ya Jiji la Taganrog itatangaza uamuzi wake kuhusu kesi iliyochukua miezi 15 ambapo Mashahidi 16 wa Yehova wameshtakiwa kama wahalifu. Wenye mamlaka Jijini Taganrog wanawashtaki Mashahidi wa Yehova kwa kupanga na kufanya mikutano ya kidini na kuongea na watu wengine kuhusu imani yao, mambo ambayo kwa kawaida Mashahidi wa Yehova hufanya ulimwenguni pote. Ikiwa Mashahidi hao watapatikana kuwa na hatia Jijini Taganrog, uamuzi huo utatekelezwa na mamlaka zote kotekote Urusi na hivyo kuifanya imani ya Mashahidi wa Yehova kuwa uhalifu.
Vyombo vya Habari Vinaweza Kuwasiliana na:
J. R. Brown, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1 718 560 5000
Urusi: Grigory Martynov, simu +7 812 702 2691