Hamia kwenye habari

MEI 23, 2018
URUSI

Urusi Yashutumiwa Kimataifa kwa Kuwatendea Vibaya Mashahidi wa Yehova

Urusi Yashutumiwa Kimataifa kwa Kuwatendea Vibaya Mashahidi wa Yehova

Umoja wa Ulaya na Marekani umetoa maelezo kuhusiana na jinsi ambavyo serikali ya Urusi imewatendea vibaya Mashahidi wa Yehova. Maelezo hayo yanafunua uwongo wa madai ya Urusi kwamba marufuku ambayo imeipiga mashirika ya kisheria ya Mashahidi wa Yehova haiwezi kuathiri uhuru wa Shahidi mmojammoja wa kufanya ibada yake. Hata hivyo, kama Umoja wa Ulaya ulivyoeleza, “madai [hayo] ni tofauti kabisa na matendo ya [serikali ya Urusi].” Ikilinganisha madai ya Urusi na jinsi inavyowatendea Mashahidi, Marekani ilieleza kwamba ni “kinyume kabisa na madai hayo.”

Wenye mamlaka wa Urusi wamewafunga Mashahidi wanane na hivi karibuni wameanzisha uchunguzi wa makosa 12 ya uhalifu dhidi ya Mashahidi katika majiji 11. Idadi inayoongezeka ya majengo yanayotaifishwa inasababisha hofu kubwa. Hata hivyo, jambo kubwa linalohangaisha ni mateso ambayo Mkristo mmojammoja anakabili kwa sababu ya imani yake.

Umoja wa Ulaya na Marekani kwa pamoja wametoa wito kwa serikali ya Urusi iheshimu makubaliano ya uhuru wa mawazo, dhamiri, na ibada au imani.

Kiunganishi cha kupata maelezo:

https://www.osce.org/permanent-council/381820

https://www.osce.org/permanent-council/381823