Hamia kwenye habari

APRILI 12, 2017
URUSI

Ushahidi wa Ziada Watolewa Siku ya Nne ya Kusikilizwa kwa Kesi Katika Mahakama Kuu ya Urusi

Ushahidi wa Ziada Watolewa Siku ya Nne ya Kusikilizwa kwa Kesi Katika Mahakama Kuu ya Urusi

NEW YORK—Mahakama Kuu ya Shirikisho la Urusi iliendelea kwa siku ya nne kusikiliza kesi kuhusu dai la Wizara ya Haki kwamba Kituo cha Usimamizi cha Mashahidi wa Yehova nchini Urusi kifungwe. Watu wengi sana walihudhuria. Mahakama ilitangaza mapumziko baadaye alasiri, na kesi itaendelea Jumatano, Aprili 19, 2017, saa 4:00 asubuhi.

Mawakili wa Mashahidi wa Yehova walianza kwa kutoa hoja zao za kutetea Kituo cha Usimamizi, na baada ya hapo mawakili wanaoiwakilisha Wizara ya Haki wakauliza maswali ili kuchanganua hoja zilizotolewa. Kwa kutegemea ushahidi uliotolewa na mawakili wa Mashahidi wa Yehova, hakimu aliiomba Wizara ya Haki itambulishe msingi hususa wa kisheria wa kutaka kufunga Kituo cha Usimamizi cha Mashahidi wa Yehova. Mawakili wa Wizara ya Haki walishindwa kumpa hakimu jibu la ombi lake wala hawakuweza kujibu maswali mengine yaliyohusiana na hilo. Siku iliisha baada ya mashahidi wa pande zote mbili kusikilizwa.

Juma lijalo, mahakama inatazamiwa kuanza kuchanganua habari kuhusu kesi hiyo.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000

Urusi: Yaroslav Sivulskiy, +7-911-087-8009