Hamia kwenye habari

UZBEKISTAN

Maelezo Mafupi Kuhusu Uzbekistan

Maelezo Mafupi Kuhusu Uzbekistan

Mashahidi wa Yehova walianza utendaji wao nchini Uzbekistan miaka mingi kabla ya nchi hiyo kupata uhuru mwaka wa 1991. Mwaka wa 1992, Uzbekistan ilipata katiba iliyozingatia haki za msingi. Hata hivyo, inapohusu uhuru wa kuabudu, mara nyingi serikali imeshindwa kufuata kikamili yaliyomo katika katiba.

Serikali ya Uzbekistan inaendelea kukataa kusajili makutaniko ya Mashahidi wa Yehova nchini humo isipokuwa moja lililopo katika mji wa Chirchik. a Kwa sababu hiyo, mikutano yoyote ya dini itakayofanywa na Mashahidi wa Yehova nje ya Jumba la Ufalme la Chirchik inavunja sheria. Mara nyingi polisi huvuruga mikutano ya kidini inayofanywa na Mashahidi katika maeneo mengine hata ile inayofanywa katika nyumba za watu. Wenye mamlaka hao huwakamata wahudhuriaji na vitu vyao vya kibinafsi na machapisho ya kidini. Polisi wamewashikilia baadhi ya Mashahidi kwa siku kadhaa na pia wamewapiga na kuwatukana. Baadhi ya Mashahidi wamepigwa faini kubwa, wameshtakiwa kama wahalifu, na kuhukumiwa vifungo vya miaka mingi kwa sababu ya kazi yao ya kuhubiri. Kitendo cha Serikali kukataa kuwasajili kunafanya utendaji wao wa amani uonekane kuwa uhalifu.

Mashahidi wa Yehova wanaendelea na mazungumzo na wawakilishi wa serikali katika jitihada zao za kupata usajili wa makutaniko nchini Uzbekistan hasa katika eneo la Tashkent. Ikiwa Mashahidi watasajiliwa, watalindwa kwa kiasi fulani dhidi ya ubaguzi wa kidini na pia uhuru wao wa ibada utaheshimiwa.

a Ilisajiliwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1994 na kusajiliwa tena mwaka wa 1999.