Hamia kwenye habari

AGOSTI 10, 2015
ZIMBABWE

Mashahidi Nchini Zimbabwe Wafanya Makusanyiko ya Mwaka 2015 yenye Kichwa “Mwigeni Yesu” Mwaka Mmoja Baada ya Kusanyiko la Kimataifa la Kihistoria

Mashahidi Nchini Zimbabwe Wafanya Makusanyiko ya Mwaka 2015 yenye Kichwa “Mwigeni Yesu” Mwaka Mmoja Baada ya Kusanyiko la Kimataifa la Kihistoria

HARARE, Zimbabwe—Mashahidi wa Yehova Nchini Zimbabwe wameanza Makusanyiko ya Eneo ya mwaka wa 2015 yenye kichwa “Mwigeni Yesu!” Ijumaa, Julai 31. Makusanyiko hayo ya siku tatu yamepangwa kufanywa kwa majuma 12 mfululizo mpaka kufikia katikati ya mwezi wa Oktoba.

Geoffrey Jackson, mshiriki wa Baraza Linaloongoza, akitoa hotuba inayotegemea Biblia katika kusanyiko la kimataifa nchini Zimbabwe mwaka wa 2014. Pembeni yake ni Mashahidi wawili wenyeji wanaotafsiri wakati uleule hotuba yake katika lugha nyingine.

Msemaji wa Mashahidi wa Yehova nchini Zimbabwe, John Hunguka alisema, “Tuna hamu kubwa ya kuhudhuria kusanyiko la mwaka huu, hasa kwa sababu ya itikio zuri tulilopata kwenye kusanyiko la pekee katika historia ya Mashahidi wa Yehova hapa nchini, yaani kusanyiko la kimataifa tulilofanya mwaka wa 2014 mjini Harare.” NewsDay, moja kati ya gazeti maarufu nchini Zimbabwe liliripoti kwamba kusanyiko hilo la kimataifa lilikuwa “kusanyiko kubwa zaidi la dini kuwahi kufanywa” nchini na lilifanya Mashahidi wa Yehova wawe miongoni mwa “watu ambao habari zao ziliongoza kutajwa na kuandikwa katika nchi hiyo” mwaka wa 2014.

Watu zaidi ya 82,000 walihudhuria siku ya mwisho ya kusanyiko la mwaka 2014, lililofanywa katika Uwanja wa Michezo wa Taifa jijini Harare. Katika mahojiano yaliyofanywa baada ya kusanyiko, John Jubber, mwakilishi wa ofisi ya tawi ya Mashahidi nchini Zimbabwe, alisema hivi: “Tulikuwa na wajumbe 3,500 kutoka Brazili, Ujerumani, Marekani, Zambia, na Kenya.”

Mwaka huu, Mashahidi wa nchini Zimbabwe wanafanya Makusanyiko ya Eneo 39 ya “Mwigeni Yesu!” katika maeneo kadhaa kutia ndani Viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Zimbabwe. Programu itasikika ikiwa nzima au kwa sehemu katika Kichina (Mandarin), Chitonga (Zimbabwe), Kiingereza, Kindebele (Zimbabwe), Kishona, Kiswahili, na Lugha ya Ishara ya Zimbabwe. Ili kujua tarehe hususa na eneo la kila kusanyiko nchini Zimbabwe tembelea tovuti rasmi ya Mashahidi ya jw.org/sw.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

J. R. Brown, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1 718 560 5000+1 718 560 

Zimbabwe: John Hunguka, simu +263 4 2910591