Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Aprili 6-12

Jumanne, Aprili 7, 2020​—Ukumbusho wa Kifo cha Kristo

Aprili 6-12

Kila mwaka katika majira ya Ukumbusho, Wakristo wengi hutafakari kuhusu upendo ambao Yehova Mungu na Mwana wake, Yesu Kristo, walionyesha. Hayo ndiyo maonyesho mawili makuu zaidi ya upendo ambayo wanadamu wamewahi kuonyeshwa. (Yoh 3:16; 15:13) Unaweza kutumia chati hii kulinganisha masimulizi ya vitabu vya Injili kuhusu huduma ya mwisho ya Yesu kule Yerusalemu. Matukio hayo yanazungumziwa katika sehemu ya 6 ya kitabu Yesu—Njia, Kweli, na Uzima. Upendo wa Mungu na wa Kristo utakuchocheaje?—2Ko 5:14, 15; 1Yo 4:16, 19.

HUDUMA YA MWISHO YA YESU KULE YERUSALEMU

Wakati

Mahali

Tukio

Mathayo

Marko

Luka

Yohana

33, Nisani 8 (Aprili 1-2, 2020)

Bethania

Yesu awasili siku sita kabla ya Pasaka

 

 

 

11:55– 12:1

Nisani 9 (Aprili 2-3, 2020)

Bethania

Maria ammiminia Yesu mafuta kichwani na miguuni

26:6-13

14:3-9

 

12:2-11

Bethania-Bethfage-Yerusalemu

Aingia Yerusalemu kwa ushindi, akiwa juu ya punda

21:1-11, 14-17

11:1-11

19:29-44

12:12-19

Nisani 10 (Aprili 3-4, 2020)

Bethania-Yerusalemu

Aulaani mtini; alisafisha hekalu tena

21:18, 19; 21:12, 13

11:12-17

19:45, 46

 

Yerusalemu

Makuhani wakuu na waandishi wapanga njama ya kumuua Yesu

 

11:18, 19

19:47, 48

 

Yehova azungumza; Yesu atabiri kifo chake; kutoamini kwa Wayahudi kwatimiza unabii wa Isaya

 

 

 

12:20-50

Nisani 11 (Aprili 4-5, 2020)

Bethania-Yerusalemu

Somo la mtini ulionyauka

21:19-22

11:20-25

 

 

Yerusalemu, hekalu

Mamlaka yake yatiliwa shaka; mfano wa wana wawili

21:23-32

11:27-33

20:1-8

 

Mifano ya: wakulima wauaji wa shamba la mizabibu, karamu ya ndoa

21:33–22:14

12:1-12

20:9-19

 

Ajibu maswali kumhusu Mungu na Kaisari, ufufuo, sheria iliyo kuu zaidi

22:15-40

12:13-34

20:20-40

 

Auuliza umati ikiwa Kristo ni mwana wa Daudi

22:41-46

12:35-37

20:41-44

 

Ole kwa waandishi na Mafarisayo

23:1-39

12:38-40

20:45-47

 

Aona mchango wa mjane

 

12:41-44

21:1-4

 

Mlima wa Mizeituni

Ataja ishara ya kuwapo kwake wakati ujao

24:1-51

13:1-37

21:5-38

 

Mifano ya mabikira kumi, talanta, kondoo na mbuzi

25:1-46

 

 

 

Nisani 12 (Aprili 5-6, 2020)

Yerusalemu

Viongozi Wayahudi wapanga njama ya kumuua

26:1-5

14:1, 2

22:1, 2

 

Yuda apanga jinsi atakavyomsaliti

26:14-16

14:10, 11

22:3-6

 

Nisani 13 (Aprili 6-7, 2020)

Akiwa Yerusalemu na maeneo ya karibu

Matayarisho ya Pasaka ya mwisho

26:17-19

14:12-16

22:7-13

 

Nisani 14 (Aprili 7-8, 2020)

Yerusalemu

Ala Pasaka pamoja na mitume wake

26:20, 21

14:17, 18

22:14-18

 

Awaosha mitume wake miguu

 

 

 

13:1-20

Yesu amtaja Yuda kuwa msaliti kisha amfukuza

26:21-25

14:18-21

22:21-23

13:21-30

Aanzisha Mlo wa Jioni wa Bwana (1Ko 11:23-25)

26:26-29

14:22-25

22:19, 20, 24-30

 

Atabiri kwamba Petro atamkana na mitume watatawanyika

26:31-35

14:27-31

22:31-38

13:31-38

Aahidi kumtuma msaidizi; mfano wa mzabibu wa kweli; atoa amri ya kupendana; sala ya mwisho pamoja na mitume wake

 

 

 

14:1–17:26

Gethsemane

Maumivu makali kwenye bustani; Yesu asalitiwa na kukamatwa

26:30, 36-56

14:26, 32-52

22:39-53

18:1-12

Yerusalemu

Ahojiwa na Anasi; ahojiwa na Kayafa, Sanhedrini; Petro amkana

26:57–27:1

14:53–15:1

22:54-71

18:13-27

Yuda msaliti ajinyonga (Mdo 1:18, 19)

27:3-10

 

 

 

Mbele ya Pilato, kisha Herode, na kurudi kwa Pilato

27:2, 11-14

15:1-5

23:1-12

18:28-38

Pilato ataka kumwachilia lakini Wayahudi wasema wanamtaka Baraba; ahukumiwa kuuawa kwenye mti wa mateso

27:15-30

15:6-19

23:13-25

18:39–19:16

(Karibu saa 9:00 alasiri)

Golgotha

Afa kwenye mti wa mateso

27:31-56

15:20-41

23:26-49

19:16-30

Yerusalemu

Mwili wake watolewa mtini na kuwekwa kaburini

27:57-61

15:42-47

23:50-56

19:31-42

Nisani 15 (Aprili 8-9, 2020)

Yerusalemu

Makuhani na Mafarisayo waweka walinzi kulilinda kaburi na kulitia muhuri

27:62-66

 

 

 

Nisani 16 (Aprili 9-10, 2020)

Yerusalemu na maeneo ya karibu; Emau

Yesu afufuliwa; awatokea wanafunzi mara tano

28:1-15

16:1-8

24:1-49

20:1-25

Baada ya Nisani 16

Yerusalemu; Galilaya

Awatokea wanafunzi wake tena na tena (1Ko 15:5-7; Mdo 1:3-8); awafundisha; awatuma kufanya wanafunzi

28:16-20

 

 

20:26–21:25