Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | MATHAYO 18-19

Uwe Mwangalifu Usijikwaze na Usiwakwaze Wengine

Uwe Mwangalifu Usijikwaze na Usiwakwaze Wengine

Yesu alitumia mifano kufundisha jinsi lilivyo jambo zito kukwazwa au kuwakwaza wengine.

18:6, 7

  • “Kikwazo” kinamaanisha tendo au hali inayomwongoza mtu kufuata njia isiyofaa, kujikwaa au kuanguka kimaadili, au kuanguka katika dhambi

  • Ingekuwa afadhali kwa mtu anayemfanya mwingine akwazike kuanguka baharini akiwa amefungwa jiwe la kusagia shingoni

Mawe ya kusagia

18:8, 9

  • Yesu aliwashauri wafuasi wake waondoe hata kitu kilicho na thamani kama mkono au jicho ikiwa linawafanya wakwazike

  • Afadhali kuacha kitu tunachopenda sana ili tuingie katika Ufalme wa Mungu badala ya kukishikilia na hatimaye tutupwe Gehena, inayowakilisha uharibifu wa kudumu

Ni nini maishani mwangu ambacho kinaweza kuwa kikwazo, na ninaweza kuepukaje kujikwaza mwenyewe au kuwakwaza wengine?