Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | MWANZO 27-28

Yakobo Apata Baraka Aliyostahili

Yakobo Apata Baraka Aliyostahili

27:6-10, 18, 19, 27-29

Isaka alitimiza unabii alipombariki Yakobo.

  • 27:28—Yehova aliwapa wazao wa Yakobo nchi yenye rutuba “inayotiririka maziwa na asali.”—Kum 26:15

  • 27:29—Waisraeli (wazao wa Yakobo) wakawa wenye nguvu zaidi ya Waedomu (wazao wa Esau).—Mwa 25:23; 2Sa 8:14

  • 27:29—Kwa chuki waliyokuwa nayo kuelekea Waisraeli, Waedomu walilaaniwa na hatimaye taifa hilo likaangamizwa.—Eze 25:12-14