Juni 17-23
ZABURI 51-53
Wimbo 89 na Sala | Utangulizi (Dak. 1)
1. Mambo Unayoweza Kufanya Ili Kuepuka Dhambi Nzito
(Dak. 10)
Usijiamini kupita kiasi—wanadamu wote wana mwelekeo wa kutenda dhambi (Zb 51:5; 2Ko 11:3)
Dumisha ratiba nzuri ya kiroho (Zb 51:6; w19.01 15 ¶4-5)
Pambana uepuke mawazo na tamaa chafu (Zb 51:10-12; w15 6/15 14 ¶5-6)
2. Hazina za Kiroho
(Dak. 10)
-
Zb 52:2-4—Mistari hii inatuambia nini kuhusu matendo ya Doegi? (it-1 644)
-
Ungependa kushiriki nasi hazina gani kutoka kwenye usomaji wa Biblia wa juma hili?
3. Usomaji wa Biblia
(Dak. 4) Zb 51:1-19 (th somo la 12)
4. Kuanzisha Mazungumzo
(Dak. 2) MAHUBIRI YA UMMA. (lmd somo la 7 jambo kuu la 3)
5. Kuanzisha Mazungumzo
(Dak. 2) NYUMBA KWA NYUMBA. (lmd somo la 4 jambo kuu la 4)
6. Kufuatia Upendezi
(Dak. 3) MAHUBIRI YASIYO RASMI. Mfundishe jina la Mungu. (lmd somo la 9 jambo kuu la 5)
7. Kufanya Wanafunzi
Wimbo 115
8. Mambo ya Kufanya Ili Kurekebisha Makosa Yako
(Dak. 15) Mazungumzo.
Licha ya jitihada nyingi, sisi sote hufanya makosa. (1Yo 1:8) Tunapokosea hatupaswi kuruhusu aibu au woga wa kuadhibiwa utuzuie kumwomba Yehova msamaha na msaada. (1Yo 1:9) Jambo la kwanza tunalopaswa kufanya ili kurekebisha kosa ni kusali kwa Yehova.
Soma Zaburi 51:1, 2, 17. Kisha waulize wasikilizaji:
-
Maneno ya Daudi yanaweza kutuchocheaje kutafuta msaada wa Yehova tunapotenda dhambi nzito?
Onyesha VIDEO Maisha Yangu ya Utineja—Ninaweza Kurekebishaje Makosa Yangu? Kisha waulize wasikilizaji:
-
Ni mambo gani ambayo yaliwaongoza Thalila na José kufanya makosa?
-
Walichukua hatua zipi ili kurekebisha makosa yao?
-
Walinufaikaje walipofanya hivyo?
9. Funzo la Biblia la Kutaniko
(Dak. 30) bt sura ya 11 ¶5-10, sanduku uk. 89