Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Utangulizi

Utangulizi

Masomo Sita Muhimu ya Kuwafundisha Watoto

Ungependa mtoto wako ajulikane kuwa mtu wa namna gani atakapokuwa mtu mzima?

  • Mtu anayejidhibiti

  • Mnyenyekevu

  • Mstahimilivu

  • Mwajibikaji

  • Mwenye akili ya utu uzima

  • Mnyoofu

Watoto hawawezi kusitawisha sifa hizo kwa uwezo wao wenyewe tu. Wanahitaji mwongozo wako.

Gazeti hili linazungumzia masomo sita muhimu ya kumfundisha mtoto wako ili kumwandaa kwa ajili ya maisha ya baadaye.