UNAWEZA KUKABILIANA NA MKAZO—JINSI GANI?
Maisha Bila Mkazo Yanawezekana
Hekima inayopatikana katika Biblia inaweza kutusaidia kuepuka kuwa na mkazo kupita kiasi. Wanadamu hawawezi kuondoa kila kitu kinachosababisha mkazo. Lakini Muumba wetu ana uwezo wa kuondoa. Amemchagua Yesu Kristo ambaye anaweza kutusaidia tunapokabili mkazo. Hivi karibuni, atafanya mambo mazuri zaidi ulimwenguni pote kuliko yale aliyofanya alipokuwa hapa duniani. Kwa mfano:
YESU ATAPONYA WAGONJWA.
“Nao wakamletea wote waliokuwa na magonjwa mbalimbali . . . , naye akawaponya.” —MATHAYO 4:24.
YESU ATAANDAA CHAKULA NA MAKAZI KWA WATU WOTE.
“[Wale watakaotawaliwa na Kristo] watajenga nyumba na kuishi ndani yake, nao watapanda mashamba ya mizabibu na kula matunda yake. Hawatajenga na mtu mwingine akae ndani yake, wala hawatapanda na watu wengine wale.”—ISAYA 65:21, 22.
UTAWALA WA YESU UTALETA AMANI NA USALAMA ULIMWENGUNI POTE.
“Katika siku zake mwadilifu atasitawi, na amani itakuwa nyingi mpaka mwezi utakapokuwa haupo tena. Atakuwa na raia kutoka bahari mpaka bahari na kutoka Mto Efrati mpaka kwenye miisho ya dunia. . . . Maadui wake wataramba mavumbi.”—ZABURI 72:7-9.
YESU ATAKOMESHA UKOSEFU WA HAKI.
“Atamhurumia mtu wa hali ya chini na maskini, naye ataokoa uhai wa maskini. Atawaokoa kutoka katika ukandamizaji na ukatili.”—ZABURI 72:13, 14.
YESU ATAKOMESHA MATESO NA KIFO.
“Kifo hakitakuwapo tena, wala maombolezo wala kilio wala maumivu hayatakuwapo tena.” —UFUNUO 21:4.