Elementi ya Ajabu
“Hakuna elementi iliyo muhimu zaidi katika uhai kama kaboni,” kinaelezea kitabu Nature’s Building Blocks. Muundo wa kaboni huiwezesha kuungana yenyewe na pia na kemikali nyingine nyingi, hivyo kufanyiza mamilioni ya miungano tata, na mingi kati ya miungano hiyo bado haijagunduliwa au kujulikana.
Mifano ifuatayo inaonyesha, jinsi atomu za kaboni zinavyoweza kuungana na kutokeza maumbo ya aina mbalimbali, kama vile minyororo, piramidi, pete, mabamba, na mirija. Kwa kweli, kaboni ni elementi ya ajabu!
ALMASI
Atomu za kaboni zinapoungana hutokeza piramidi ziitwazo tetrahedron, zilizo na umbo imara na hufanya almasi kiasili iwe ngumu kuliko kitu chochote. Kimsingi almasi halisi ni molekuli iliyofanyizwa na atomu za kaboni.
GRAFITI
Ni tabaka la atomu za kaboni zilizoungana na kujipanga kwa kuachiana nafasi kwa njia inayoweza kupekuliwa kama kurasa za kitabu. Kwa hiyo grafiti ni laini na ni muhimu katika utengezaji wa penseli. *
GRAFATI
Ni tabaka moja la atomu za kaboni lenye mpangilio wenye matundu yenye umbo la pembe sita. Grafati ni imara zaidi kuliko chuma. Ncha ya penseli inaweza kuwa na kiasi kidogo cha grafati katika tabaka moja au zaidi.
MOLEKULI ZA FULLERENE
Hizi ni molekuli za kaboni zenye mashimo na umbo la mviringo kama mpira na zingine zenye umbo la mirija zinazoitwa nanotube. Hupimwa katika nanometa, au mabilioni ya meta.
VIUMBE HAI
Chembe nyingi zinazofanyiza mimea, wanyama, na mwanadamu zinatokana na kaboni, yaani, elementi inayopatikana katika kabohaidreti, mafuta, na amino asidi.
“Sifa za [Mungu] ambazo hazionekani . . . zinaeleweka kwa vitu vilivyofanywa.”—Waroma 1:20.
^ fu. 7 Soma makala “Naomba Penseli?” katika gazeti la Amkeni! la Julai 2007