Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

La Bambouseraie Mradi Uliotimizwa

La Bambouseraie Mradi Uliotimizwa

La Bambouseraie Mradi Uliotimizwa

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA UFARANSA

YAPATA miaka 150 iliyopita huko kusini ya Ufaransa, Eugène Mazel, mnunuzi wa vikolezo kutoka Asia, alianzisha bustani ya miche ya mwanzi ambayo ingekuwa kubwa zaidi ulimwenguni, yenye namna 200 hivi ya mmea huu unaokua haraka na wenye matumizi mengi. Kufikia mwaka wa 1855, tamaa ya Mazel ilikabili kizuizi kikubwa: Mwanzi haukukua Ulaya.

Jitihada za kuleta mmea huo kutoka Asia hazikufua dafu. Ingawa mwanzi husitawi katika mazingira yake (aina fulani inaweza kustahimili halijoto ya kiwango cha chini cha nyuzi –24 Selsiasi na inaweza kukua kwenye mwinuko wa meta 5,000), haikuwezekana kudumisha mizizi ikiwa hai wakati wa safari ndefu ya kuvuka mabara. Hata hivyo, baada ya kutokea kwa meli zenye mwendo wa kasi zaidi, sampuli za mianzi zilipelekwa Uingereza kwa mafanikio mwaka wa 1827 na, baadaye, huko Ufaransa. Mradi wa Mazel ulikaribia kuwa halisi!

Kisha Mazel akakabili ugumu wa kupata mahali panapofaa kwa ajili ya bustani yake ya miche. Mnamo mwaka wa 1855 alinunua shamba la ekari 84 karibu na Anduze, kusini ya Ufaransa, lililokuwa na tabia ya nchi ya Mediterania na udongo uliofaa. Kazi nyingi sana ililazimika kufanywa ili kuelekeza maji kutoka kwenye mto uliokuwa karibu. Lakini jitihada zenye bidii za Mazel zilifanikiwa.

Kwa kusikitisha, kufikia mwaka wa 1890, Mazel alifilisika na akalazimika kuuza shamba lake lenye thamani. Hata hivyo, jambo la kufurahisha ni kwamba wengine waliendelea kutoka mahali alipoachia, hivi kwamba sasa kila mwaka watu wapatao 350,000 huzuru La Bambouseraiemradi wa Mazel uliotimizwa.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 31]

Picha zote: La Bambouseraie de Prafrance